Muigizaji na mwimbaji wa Marekani akutwa amekufa nyumbani kwake
Maafisa wa Los Angeles, Marekani wameeleza kuwa mwimbaji na muigizaji wa kike Simone Battle amekutwa nyumbani kwake akiwa amefariki, Ijumaa asubuhi.
Battle aliwakuwa muigizaji na mwimbaji wa kundi la pop la G.R.L, ambaye alifika katika hatua ya fainali ya shindano la kuimba la X Factors mwaka 2011.
Polisi walieleza kuwa mwili wake utafanyiwa uchunguzi Jumapili (jana) ili kufahamu chanzo cha kifo chake.
Angalia video ya wimbo wa Simone 'He Likes Boys' alifanya mwaka 2011.
Post a Comment