Lupita Nyong'o kuigiza simulizi la mwandishi wa kike wa Nigeria
Lupita Nyong’o amepewa nafasi ya kuigiza filamu yenye simulizi la novel maarufu ya ‘Americanah’ iliyoandikwa na mwandishi wa Nigeria mwenye heshima kubwa Afrika kutokana na kazi yake, Chimamanda Ngozi Adichie.
Americanah itashutiwa na kampuni ya Plan B ya Brad Pitt ambayo ilimpa nafasi Lupita kuigiza kwenye 12 Years A Slave iliyompa sifa na tuzo kubwa.
Muigizaji huyo wa Kenya ambaye ni mshindi wa tuzo za Oscar anapewa nafasi hiyo siku chache baada ya kutangazwa kuwa atashiriki kwenye filamu maarufu duniani ya ‘Star Wars’ Episode VII akiungana na waigizaji wengine wakubwa .
Americanah ni moja kati ya kazi nzuri za Chimamanda Ngozi Adichie ambazo zinawekwa kwenye orodha ya vitabu bora alivyowahi kuandika pamoja na Purple Hibiscus na Half of Yellow Sun.
Post a Comment