toqeer toqeer Author
Title: Jennifer Lopez ajitoa kufanya onyesho katika ufunguzi kombe la Dunia
Author: toqeer
Rating 5 of 5 Des:
Mwanamuziki Jennifer Lopez ambaye alitakiwa kuimba wimbo maalum katika sherehe za ufunguzi wa mashindano ya mwaka huu ya kombe la dunia nc...
JLOMwanamuziki Jennifer Lopez ambaye alitakiwa kuimba wimbo maalum katika sherehe za ufunguzi wa mashindano ya mwaka huu ya kombe la dunia nchini Brazil amejitoa kufanya onyesho hilo.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa mwanamuziki huyo, Jennifer Lopez hatashiriki sherehe za mwaka huu za ufunguzi wa kombe la dunia ambapo hajatoa sababu ya kufikia uamuzi huo.
Lopez aliungana na rapa Pitbull pamoja na nyota wa nchini Brazil Claudia Leitte kwa ajili ya kurekodi wimbo maalum wa kombe la dunia kwa mwaka huu uliopewa jina la “We Are One (Ola Ola).”
Wanamuziki hao watatu kwa pamoja walitakiwa kuimba wimbo huo katika sherehe za ufunguzi katika mechi ya kwanza lakini Jlo amesitisha na kusema hatokuwepo tena.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top